faida za mfumo

img

Suluhisho Letu

Smart Finance si tu mfumo wa kawaida kama ilivyo mifumo mingine; ni mfumo wa kidigitali ambao unaunganisha urahisi, ufanisi, na udhibiti wa hali ya juu.

Zifuatazo ni baadhi ya sifa kuu ambazo Smart Finance inakuletea:

Security Icon

Usalama wa Taarifa

Smart Finance hutoa uhakika wa usalama wa taarifa kwa kutumia teknolojia za hali ya juu za kielektroniki na mifumo thabiti ya uhifadhi wa data.

Security Icon

Usaidizi wa Kifedha

Smart Finance inatoa uwezo wa kufanya malipo na shughuli nyingine kupitia simu za mkononi, ikirahisisha sana mchakato wa kifedha kwa wanachama.

Security Icon

Urahisi wa Matumizi

Mfumo wa Smart Finance ni rahisi sana kutumia na unaeleweka haraka, hivyo kuongeza ufanisi na kuondoa kero za kiutawala.

img


img


img

Icon Usimamizi wa Mikopo na Fedha

  1. Kuingiza mikopo na kufanya marejesho kwa njia rahisi na ya kidigitali.
  2. Kufanya mahesabu ya riba na kufuatilia marejesho kwa usahihi.
  3. Kupata taarifa za kina kuhusu hali ya mikopo na uwezo wa wanachama kurudisha fedha.
  4. Kuweza kusimamia matawi yako mbalimbali katika mfumo mmoja na kwa urahisi zaidi huku kila tawi likiona taarifa zinazoihusu tu bila kuvuruga za tawi lingine.

Icon Utunzaji wa Kumbukumbu

  1. Kuhifadhi rekodi sahihi za mikopo, hisa, amana, na akiba kwa kila mwanachama/mteja
  2. Kutoa taarifa za kina za kifedha kwa kila mwanachama/mteja, kwa kila bidhaa.
  3. Kutoa ripoti za mikopo, deni la mteja, marejesho ya mkopo, miamala ya mikopo, na taarifa za hisa, amana, na akiba.

Icon Uwepo wa App ya Simu (Mobile Application)

  1. Mfumo unaambatana na programu ya simu (Mobile Application) ambayo inatoa ufikiaji rahisi na wa haraka kwa taarifa za miamala na Kiasi cha mikopo, hisa, amana, na akiba kwa wanachama.
  2. Wanachama wanaweza kufuatilia taarifa zao za kifedha popote walipo na wakati wowote kupitia simu zao za mkononi, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa taarifa kwa urahisi na ufanisi.
  3. Programu ya simu inaruhusu wanachama kufanya marejesho ya mikopo yao na kuongeza akiba zao moja kwa moja kupitia programu hiyo wakiwa mahali popote.
  4. Hii hupunguza urasimu na muda wa kusafiri kwenda benki au matawi ya ushirika kufanya miamala hiyo, huku ikiongeza urahisi katika usimamizi wa fedha za wanachama.
  5. Uwezo wa mwanachama / mteja kufanya maombi ya mkopo moja kwa moja kwa kutumia app yake ya simu ya mkononi na kuweza kuambatanisha nyaraka za mkopo zinazotakiwa.

Icon Usimamizi wa Nyaraka

  1. Kuweka nyaraka muhimu kama maombi ya mikopo, mikataba, dhamana ya mikopo na nyaraka za usajili katika mfumo wa kidigitali
  2. Kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu na upatikanaji wa taarifa kwa wepesi zaidi.

Icon Upatikanaji wa Taarifa za Kifedha

  1. Kutoa ripoti za kina kuhusu hali ya kifedha ya taasisi yako, ikiwa ni pamoja na ripoti za mikopo, amana, hisa, na akiba.
  2. Kurahisisha ufuatiliaji wa miamala na hali ya kifedha kwa ufanisi zaidi

Icon Uwezo wa Kiuhasibu

  1. Kutoa taarifa mbalimbali za uhasibu kama ripoti za mapato na matumizi, miamala ya leja kuu, na hata mchanganuo wa kifedha kama taarifa ya mizania, taarifa ya mtiririko wa fedha, taarifa ya mabadiliko ya mtaji pamoja na maelezo ya kina kuhusu mahesabu (Accounting Notes), taarifa ya miamala ya leja kuu, usuluhisho wa kibenki, taarifa ya ulali na usawa, na taarifa nyinginezo zinazosaidia katika usimamizi mzuri wa fedha na uhasibu.
  2. Uwezo wa Kutoa Taarifa za tume (TCDC reports) za kila mwezi na za kila robo ya mwaka zinazosaidia katika kufanya maamuzi ya kimkakati kwa SACCOS.
  3. Uwezo wa Kutoa Taarifa za Benki Kuu (BoT reports) kama inavyotakiwa na benki kuu kufuata mwongozo wake

Icon Usimamizi wa Rasilimali Watu na Mishahara

  1. Uwezo wa kufanya mahesabu ya mishahara na kutoa pay slips kwa wafanyakazi wote.
  2. Huduma za rasilimali watu kama vile kuomba likizo moja kwa moja kwa njia ya kidigitali kupitia kwenye mfumo na kutunza nyaraka za wafanyakazi na mikataba ya ajira.

Icon Uwezo wa kuunganishwa na Mabenki na Makampuni
ya Simu pamoja na Mifumo Mingine
(Bank and Other Systems Integration)

  1. Uwezo wa kuunganishwa na mifumo ya malipo ya makampuni ya kifedha kama benki na makampuni ya simu, pamoja na uwezo wa kuunganishwa na mfumo wa tume ya vyama vya ushirika (TCDC) kama vile MUVU.
  2. Huduma za malipo kupitia simu ya mkononi na uwezo wa kufanya miamala kwa urahisi kupitia simu yako ya kiganjani.

Icon Ufuatiliaji na Mawasiliano na Wateja:

  1. Uwezo wa wateja kuona taarifa za mikopo, hisa, amana, na akiba kupitia simu zao za mkononi.
  2. Ujumbe mfupi (SMS) kwa wateja kuhusu miamala yao na taarifa muhimu kama vile heri ya sikukuu na ukumbusho wa marejesho.

Icon Uwezo wa Kurekodi Miamala moja kwa moja

  1. Malipo yanayofanyika kwa njia ya simu/bank yanajirekodi moja kwa moja kwenye mfumo, kurahisisha usimamizi wa kifedha na kupunguza makosa ya kunakiri.
  2. Mfumo una uwezo wa kutuma ujumbe wa SMS moja kwa moja baada ya mteja kulipia deni lake au kuweka akiba/amana/hisa yake, pamoja na kutoa taarifa ya historia ya miamala yako yote ambayo umewahi kufanya.